Upimaji wa Utendaji Kazi Sashin Shaidar

Upimaji wa Utendaji Kazi. Katibu Mkuu wa Wizara, Mkuu wa Idara Inayojitegemea, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri husika, Mkurugenzi wa Uhamiaji na Kamishna wa Zimamoto na Huduma za Uokoaji watakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa watumishi walio chini yao wanapimwa utendaji kazi wao kwa kuzingatia malengo ya kazi kama yalivyoainishwa katika Mikataba ya Utendaji Kazi (Performance Contract) ya watumishi hao. Katika utaratibu huu, Watendaji Wakuu watapimwa utendaji kazi wao kwa kuzingatia utaratibu ufuatao: -