OFISI YA WAKIMBIZI WA JIMBO LA NORTH CAROLINA MAKUBALIANO YA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA WAKIMBIZI
OFISI YA WAKIMBIZI WA JIMBO LA NORTH CAROLINA MAKUBALIANO YA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA WAKIMBIZI
Xxxx, , ninakubaliana na MASHARTI yafuatayo ya (shirika) huduma za ajira:
Ninakubaliana kufuata Makubaliano yangu ya Uwajibikaji wa Pamoja (MRA, Mutual Responsibility Agreement) na Mpango wa Utekelezaji.
Nitajiandikisha kwa huduma za ajira na (shirika).
Ninakubali kushiriki katika mpango wowote wa uwezo wa kuajiriwa unaotolewa kupitia huduma za (shirika) ajira ambazo zinatoa mafunzo ya kazi, mafunzo ya lugha, au ujuzi mwingine wa ajira.
Nitahudhuria miadi yote iliyopangwa na wafanyakazi wa (shirika) huduma za ajira. Ikiwa siwezi kuhudhuria miadi, nitawasiliana na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira angalau masaa mawili kabla ya miadi iliyopangwa.
Ninakubali kushiriki katika mahojiano yoyote ya kazi yatakayoandaliwa na wafanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
Nitakubali ajira yoyote inayopatikana iliyobainishwa kuwa inafaa na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
Ikiwa nitakubali ajira nje ya huduma za (shirika) ajira, nitawasiliana mara moja na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
Baada ya kukubali ajira, nitaenda kazini katika tarehe ya kuanza kazi iliyokubaliwa wakati wa ajira.
Kabla ya kuacha kazi, nitazungumza na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
Nitawasiliana na ofisi ya (shirika) huduma za ajira mara moja ikiwa tatizo litatokea, au ikiwa xxxx xxxxxxxxxx ambayo yananizuia kushiriki katika shughuli zilizoandikwa katika MRA hii. Nisipotii MRA inaweza kusababisha kupunguzwa au kukomeshwa kwa huduma za (shirika) ajira.
Sitaacha kazi kwa hiari bila sababu nzuri.
Ninaelewa kwamba, ikiwa nitaacha kazi kwa hiari au sitafuata Makubaliano yangu ya Uwajibikaji wa Pamoja, nitasimamishwa kushiriki katika huduma za (shirika) ajira.
Ikiwa nitaacha kazi kwa hiari au sitafuata Makubaliano yangu ya Uwajibikaji wa Pamoja, ninaelewa kwamba ni lazima nitekeleze Mpango wa Utekelezaji kabla ya huduma za ajira kurejeshwa.
Ikiwa nitaacha kazi kwa hiari au sitafuata Makubaliano yangu ya Uwajibikaji wa Pamoja, ninaelewa kuwa xxxx langu litawekwa chini ya orodha ya (shirika) ya huduma za ajira hadi nitakapotekeleza Mpango wa Utekelezaji nilioundiwa na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
Ikiwa nitaacha kazi kwa hiari, kuacha xxxx xxxx taarifa, au kukataa kazi niliyopewa na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira, ninaelewa kwamba Idara ya Huduma za Jamii itajulishwa, na misaada yoyote ninayostahili kupokea inaweza kupunguzwa au kukomeshwa.
Mfanyakazi wa (shirika) Huduma za Ajira anakubali kukusaidia kupata na kudumisha kazi kwa:
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira zinazofaa, zenye mshahara unafikia au unazidi kiwango cha chini cha mshahara kilichowekwa na nchi au jimbo.
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira zenye saa za kazi za kawaida za kila siku na kila wiki.
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira unazoweza kuzifanya mara kwa mara.
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira zilizo ndani ya wakati uliokubaliwa wa usafiri kila siku, na ambazo zinaruhusu mipango yoyote muhimu ya huduma ya matunzo ya watoto.
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira na kituo cha kazi ambayo kinachotimiza viwango vyote vinavyohusika vya afya na usalama.
• Kukuelekeza tu kwa fursa za ajira ambazo sera zake haziruhusu ubaguzi kazini kwa kuzingatia umri, jinsia, asili, imani, rangi au utaifa.
• Kusaidia kupanga huduma kama vile huduma ya matunzo ya watoto, usafiri na huduma zingine kama ilivyoelezwa katika MRA yako na/au Mpango wa Utekelezaji.
• Kukuelekeza kwa huduma na nyenzo nyingine za jamii za kukusaidia uweze kujitegemea kiuchumi.
• Kutoa msaada wa mafunzo ya kazi, mafunzo ya lugha, au ujuzi mwingine wa ajira kama ilivyobainishwa na mfanyakazi wa (shirika) huduma za ajira.
• Kujadiliana nawe wakati Mpango wa Utekelezaji unahitaji kusasishwa au kubadilishwa.
• Kukupa sera hizi kwa lugha yako ya msingi, kwa tafsiri au kwa maandishi.
• Kukupa nakala ya Sera ya Kuwasilisha malalamiko ya Mpango wa Wakimbizi wa Jimbo.
Ninaelewa kinachohitajika kutoka kwangu. Ninaelewa pia kwamba huduma za (shirika) ajira zinaweza kupunguzwa au kukomeshwa ikiwa sitatii, isipokuwa ikiwa nitatoa sababu nzuri kama ilivyoelezwa katika Mwongozo/Sera ya Mpango wa Huduma za Wakimbizi. Ninaelewa pia kuwa nina haki ya kukata rufaa kuhusu hatua yoyote iliyochukuliwa na Mfanyakazi wa (shirika) Huduma za Ajira.
Mteja
(Saini) (Tarehe)
Nambari ya Mgeni
(Shirika) Mfanyakazi wa Huduma za Ajira
(Saini) (Tarehe)
Xxxx
Xxxxx ya Mkalimani au Tafsiri Imeambatishwa
MAAGIZO YA KUJAZA
OFISI YA WAKIMBIZI YA JIMBO LA NORTH CAROLINA MAKUBALIANO YA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA WAKIMBIZI
MADHUMUNI:
Madhumuni ya fomu hii ni kutoa zana ya kubainisha wazi matarajio ya wajibu wa mteja anayejiunga na mpango wa uwezo wa kuajiriwa na shirika, pamoja na wajibu wa shirika kwa mteja. Fomu hiyo inapaswa kujazwa na mfanyakazi wa shirika la wakimbizi anayehusika na mpango wa huduma za ajira. Makubaliano ya Uwajibikaji wa Pamoja yanapaswa kujumuishwa kwenye faili ya mteja pamoja na Mpango wa Uwezo wa Kuajiriwa (DSS-6232).
MAAGIZO:
- Wateja wanapaswa kubainisha kwamba wameelewa wajibu wao kama ilivyobainishwa kwenye ukurasa wa kwanza kwa kuweka herufi za kwanza za xxxx xxx kwenye kila mstari katika nafasi iliyowekwa.
- Mfanyakazi wa shirika anapaswa kufafanua wajibu wa shirika kwa mteja, na mteja anapaswa kutia saini na tarehe kwenye ukurasa wa pili, pamoja xx xxxxx na tarehe ya mfanyakazi wa shirika.
- Hakikisha mkalimani xxxxxx xxxxx fomu ya Makubaliano ya Wajibu wa Pamoja baada ya kufafanuliwa na kutafsiriwa kwa mteja (ikiwa inatumika). Ikiwa hakuna mkalimani aliyehitajika, tafadhali andika Haitumiki.
Kumbuka: Mfanyakazi wa mtoa huduma anayejaza fomu ya Makubaliano ya Wajibu wa Pamoja anapaswa kuhakikisha mteja anapata nakala iliyotiwa saini ya fomu hiyo baada ya kujazwa.