Makubaliano katika Upimaji wa Utendaji Kazi. • Iwapo panatokea kutokukubaliana kati ya msimamizi na mtumishi katika kupimwa utendaji kazi, utaratibu huu unatoa nafasi ya kumhusisha mtu wa tatu anayefahamu kwa undani kazi za eneo husika ili atoe maoni yake ambayo msimamizi na mtumishi watayachukulia maanani katika kukamilisha zoezi la upimaji utendaji kazi. • Pale ambapo hapatakuwa na makubaliano katika upimaji wa utendaji kazi kati ya msimamizi na mpimwaji msimamizi atamshauri mpimwaji kuwasiliana na mamlaka ya juu zaidi. Aidha pale ambapo hapatakuwa na makubaliano kati ya Waziri na Katibu Mkuu, Waziri atatakiwa kupata ushauri kutoka Tume ya Utumishi waUmma ambapo Tume itateua mjumbe wake ambaye atatoa ushauri. Endapo baada ya kupata ushauri bado pande hizo mbili hazitafikia makubaliano, mjumbe wa Tume atatakiwa kuandaa taarifa na mapendekezo yake na kuyawasilisha kwa Tume ambayo hatimaye itawasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwa uamuzi wa mwisho.