Mikataba ya Utendaji Kazi. Kila mtumishi wa umma atatakiwa kusaini mkataba wa utendaji kazi (Performance Contract) na msimamizi wake wa kazi mkataba ambao utajumuisha malengo waliyokubaliana pamoja na rasilimali inayohitajika ili kutekeleza malengo hayo. Pia msimamizi wa kazi husika ndiye atapima utendaji kazi wa watumishi aliosaini nao mkataba wa utendaji kazi, kwa kuzingatia malengo yaliyoainishwa katika mikataba ya utendaji kazi. Utaratibu wa kusaini mikataba ya kazi utakuwa kama ifuatavyo: