Taarifa za mwaka. Kila mtumishi wa umma ataandaa taarifa ya tathmini ya utendaji kazi kwa kila mwaka. Taarifa hiyo itajadiliwa katika kikao cha pamoja kila mwisho wa mwaka kati ya msimamizi na mtumishi ili kutathmini mafanikio na matatizo yaliyojitokeza ili kukubaliana namna ya kufanikisha malengo ya baadaye ya kazi na ya mwajiriwa katika maendeleo yake ya kazi kwa mfano kuthibitishwa kazini, kuongeza ujuzi, nyongeza ya mshahara, kupandishwa cheo na kadhalika.